Millionaire  Ads

Wednesday, August 6, 2014

WAAMUZI WA MPIRA WA MIGUU WAWAKIVUTIO KWA WADAU WA SOKA MKOANI SINGIDA

Tags

Kutokana na mikakati inayo fanywa na chama cha waamuzi wa mpira wa miguu mkoani Singida (FRAT) kumekuwa na utaratibu kabambe ulio ratibiwa na  Waamuzi wa ligi Kuu na FIFA wanaotoka Mkoa wa Singida. Chama hiki kimekuwa mfano wa kuigwa mkoani Singida. ubora huu umetokana na waamuzi kuwa na vipindi vya kufanya mazoezi kwa pamoja na pia kukaa na kupitia sheria Kumi na saba za soka kwa pamoja pia hali imepelekea chama hiki kiwe na mshikamano mzuri sana.
Wadau wa Mpira pia wameenda mbali kwa kupongeza  uongozi wa chama cha waamuzi wa soka  na Chama cha Mpira Mkoa  wa Singida.
Ikumbukwe pia chama hiki mwanzoni mwa mwaka kilipatwa pigo la kuondokewa na Mwanyekiti wachama  hayati Bw.Josephati Magazi ambaye pia alikuwa mkufunzi mkuu wa Wawaamuzi wa mpira wa miguu kwa mkoa wa Singida na  Mechi Kamishina wa ligi kuu kwa zaidi ya miaka kumi na mbili, hata hivyo kutokana na miongozo yake mizuri  waamuzi wameendelea kumuenzi kwa kushikamana na kuendelea kuwa wamoja na wenye nia ya kuhakikisha wanakuwa wadau halali wa mpira wa miguuua kwa kufuata miongozo na kanuni zinazo simamia chama.
kwa hili hongera chama cha Waamuzi mkoa wa singida na hongera waamuzi wa ligi kuu na FIFA kwa kuwa msitari wa mbele kuwaongoza waamuzi wenzenu na kuwa saidia kimazoezi.

Waamuzi wa mpira wamiguu Mkoa wa Singida wakiwa katika majadiano baada ya mazoezi  siku ya Juma mosi katika uwanja wa mkoa wa Namfua Singida.

 Waamuzi wa mpira wa miguu wakiwa katika  zoezi la kuunyosha mwili baada ya mazoezi
Picha  juu ni Darasa la waamuzi wa mpira wa miguu Mkoa wa Singida wakiwa katika mafunzo ya sheria kumi na saba za soka chini ya wa kiongozwa na Mwl. Arnold Bugado ambaye pia ni Mwamzi wa daraja la kwanza na anachezesha michezo ya Ligi kuu Tanzania bara.

2 comments

Maoni watakaopenda watachangia kama hivi mimi navyochangia. Unaandika habari nzuri sana

Changia mawazo yako hapa, Kuwa huru kuandika chochote kwa manufaa ya jamii
EmoticonEmoticon

:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:o
:>)
(o)
:p
:-?
(p)
:-s
8-)
:-t
:-b
b-(
(y)
x-)
(h)