Millionaire  Ads

Saturday, August 16, 2014

KWA HILI UONGOZI WA CCM MKOA WA SINGIDA MTUTAKE RADHI WANANCHI WENU PAMOJA NA WADAU WOTE WA MICHEZO NCHINI TANZANIA.

Tags

Nitakribani wiki mbili tangu kile kilichoisemwa na vyombo vingi vya habari nchini kuwa Mhe.Dewji Mbunge wa Jimbo la singida mjini kuwa ameamua amwandikie Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Bw.Abdulrahman Kinana kuwa kumekuwa sitofahamu  juu ya ujenzi wa Uwanja unao juklikana kama uwanja wa mkoa wa singida wa Namfua. hali hii imetokana na kukwamishwa kwa jitihada za kuufanyia ukarabati na ujenzi ikiwa ni ahadi ya Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na Mbunge wa singida Mjini Mh. Mohammed Dewji. Utata huo umetokea baada ya uongozi wa chama cha mapinduzi Mkoa wa singida kutoruhusu Mchakato huo kuendele kwa zaidi ya mwaka sasa kwa sababu ambazo zimekuwa hazieleweki kila siku.
kwa maelezo toka kwa moja ya wasemaji  wa kampuni ya "Mohammed enterprises" ilielezwa kwamba Kampuni hiyo imetekeleza kile kile ambacho ilitakiwa kukifanya kwa manufaa ya wananchi,  bali tatizo kubwa ni upande wa uongozi wa mkoa wa chama cha mapinduzi  na hili limetokana na kuwa uwanja wa namfua ni moja ya maeneo ambayo yanamilikiwa na chamahicho kwa mkoa wa singida hivyo basi.Raisi kwa upande wake Alifanya yake ya kutafuta fedha ambazo zilitakiwa katika ukarabati wa uwanja ambapo Kampuni Airtel ilikubali kutoa fedha Jumla ya shilingi milioni Mianane  wakati mbunge wa Singida Mjini yeye kwa kupitia kampuni ya  Mohammed interprises alito fedha zaidi ya Milioni Mia sita kiasi ambacho kilionekana kinaweza kutosha walau kwa kuanzia ukarabati na ujenzi wa uwanja huo. Suala ambalo limekuwa gumu sana ni Kitendo cha Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi kutoruhusu ujenzi huu kuendele kwa mwaka moja na zaidi sasa.
  • Labda swali ambalo wote tunatakiwa tujiulize kuwa je kuna uzito gani  kuruhusu tuu, ujenzi huu uendele ikiwa fedha zipo na kampuni  ya masasi construction imekwisha kuwa tayari kufanya kazi hiyo?
  • Pia tujiulize kazi kubwa ni ipi kati ya kuruhusu uwanja  ujengwe, kujenga na kutafuta fedha za kujengea?
  • Je kama upande wa kwanza wawadhamini wa utengenezaji wa uwanja huu wamejitole kwa manufaa ya umaa! Ni kwanini chama kinatufanyia hivyo wananchi wake na  wadau wa michezo? 
  • Si hivyo tu suala jingine pia tufikirie  uwanja huu utanufaisha watu wangapi pidi utakapao kamilika?
CCM ni  chama pekee ambacho hata wadau tunakubali kuwa kimeto fursa za kuibua vipaji kwa asilimia kubwa sana nchiTanzania  kwa  hakika haya ya singida hayaendani na hadhi ya chama na pia ni mwelekeo mbaya kwa chama na maendeleo ya michezo pia.
Nafikri kama kunatofauti za kisisasa ni vizuri zikamalizwa kwa utaratibu mwingine na wala si kwa kudidimiza michezo kwani tutakuwa tuna wanyanyasa wananchi wetu ambao wanaguswa na suala zima zima la michezo.
lakini pia swala la kukumbuka na  tulikuwa tunaomba chama kifahamu nikwamba tunahuzunishwa sana kuona kuna viongozi ambao wamekuwa hawana uchungu na maendeleo ya michezo  mkoani singida   ikiwa ni moja ya mikoa ambayo imekosa hata uwakilishi wa Timu kwa mashindano ya kitaifa na kimataifa ilihali wachezaji wapo na uwezo wanao.
Haya mambo kiukweli yanaturudisha nyuma sana na tunaumia tunavyo yaona yanaendelea tena katika sura tofautitofauti kama hili la ujenzi wa kiwanja.
Tunawashukuru wadau hawa wanaoifikiria singida kuwa ibadilike kitaswira kwa upande wa michezo tunaomba wasichoke , na ndugu zetu viongozi wa CCM waone kuwa sisi tunawaona utendaji wao wa kazi na jinsi wanavyo yajali makundi mbalimbali katika jamii. sivizuri tukatanguliza masilahi ya kisiasa  kulioko maswala yanayogusa jamii kwa ujumla.
tunawaomba  mfikirie upya na kututaka radhi wadau wa michezo na wanachi wa Singida na Taifa kwa ujumla.
        Jukwa la uwanja wa Namfua

 Jukwa la upande wa mashariki ya uwanja wa Namfua

 Upande wa Goli wa kaskazini mwa uwanja wa Namfua

 Sehemu ya uwanja wa Namfua Kwa ndani
                                    
 Wanafunzi wakifanya Mazoezi Katika Uwanja wa Namfua Mwaka 2012


 Tunataka Uwanja wa Namfua ubadilike walau ufanane kidogo na uwanja huu wa Azam

Majukwa ya uwanja si vibaya yakawa  na taswira kama hii kuliko jukwa lilopo kwa saasa ambalo bati zinapiga kelele mda wote.



2 comments

kweli uwanja wetu wa Namfua haufai kabisa kweli soka la Singida ni shida sana japo kuna wachezaji wazuri sana.

kunahaja ya kukumbushana kila mmoja wetu atimize wajibu bila shuruti

Changia mawazo yako hapa, Kuwa huru kuandika chochote kwa manufaa ya jamii
EmoticonEmoticon