Millionaire  Ads

Monday, August 11, 2014

SEMINA YA WALIMU 12 WA MICHEZO KUFANYIKA MKOANI SINGIDA

Tags

Kutokana na wadau wengi kuguswa na maendeleo duni ya michezo Shuleni na mitaani Mradi wa TTU- Education Through Sports unaendesha semina ya walimu kumi na wawili ambao wanaandaliwa kuwa Walimu wa Walimu wenzao wanaofundisha michezo Mashuleni. Semina hii ni Mpango madhubuti wa kuona shule inakuwa ni chimbuko la Vipaji na Sehemu sahihi ya kuendeshea michezo kwa kuwa walimu ndio kundi pekee linalokaa na watoto tangu wakiwa wadogo hadi kukua kwao, hivyo basi mradi umeamua kuweka mkakati huo ili kuto fulsa hiyo kwa watoto.(Wanafunzi).
Meneja wa Mradi huu ameeleza kuwa anasikitishwa sana ana maendeleo Duni ya michezo Mkoa wa Singida na hata taifa kwa ujumla. amesema,
Michezo huchochea mahudhurio, Hutukinga na Magonjwa Mbalimbali hasa ya kitabia na pia hujenga Ushirikiano ndani ya jami na hata jamii moja hadi nyingine.
Sambamba na hilo amewasitiza walimu kuwa wabunifu katika uendeshaji wa ratiba zao za michezo kwani michezo huhitaji muda mwingi zaidi kuliko masomo mengine yanayo fundishwa shuleni.
Walimu nao pia katika ufunguzi wa Semina hii wameeleza kuwa bado kumekuwa na changamoto kubwa sana pindi wakiwa katika ufundishaji wa michezo  baadhi  ni
  1. Kukosa ushirikiano kutoka  kwa wakuu wa shule .
  2. Uhaba wa vifaa vya michezovya kufundishiwa.
  3. Uwepo wa masomo mengi ambayo  wanahitajika kuwafundisha zaidi ya michezo. 
  4. baadhi ya wadau kuto watambua wao pia kama wataalamu wa michezo. 
Sambamba  na hayo Mradi huu umewezesha  uwepo wa miondombinu ya kimichezo kwa Mkoa mzima  Singida kwa  upande wa Shule za Msingi na Sekondari. kutokana na taarifa ya Mradi huo wa TTU- Education Through Sports imeelezwa kuwa Mradi umegawa magoli ya chuma  ya Mpira wa miguu, Mpira wa Wavu na Mpira wa Netiboli kwa shule zote za Mkoa wa Singida Sekondari na Msingi.
Semina hii itafanyika  kwa Muda wa siku tano hivyo tutaendele kujuzana  kila kitakacho kuwa kikiendelea katika semina hii.

    Mwl. Arnold Bugado ambaye pia ni Meneja wa mradi akijadili na walimu wa michezo jinsi ya     kuandaa mikakati na namna nzuri ya kufundisha michezo ki-utaalamu.


 Wanasemina Wakiendelea na Mafunzo Katika  Ukumbi wa Jengo La chama cha Walimu Mkoa wa Singida.



Changia mawazo yako hapa, Kuwa huru kuandika chochote kwa manufaa ya jamii
EmoticonEmoticon