Millionaire  Ads

Monday, August 4, 2014

HONGERA MPOMBO CUP

Tags

Nitakribani mwezi mmomja  sasa tangu  ligi ya mpira wa miguu  ianze  Wilaya ya Singida vijijini, hongera sana Bwana Mpombo kwa maono yako mazuri ya kuvaa jukumu la kuendeleza michezo mkoani singida. Ligi hii ni kubwa sana kwa mkoa huu wa singida kwani inakaribia kuwa na timi zaidi ya thelathini. Nimatumaini ya kila mwana Singida  kuwa kwa mwendo huu  kuna taswira  nzuri siku za usoni kwa Mkoa na hata Taifa kwa ujumla.

 Ushauri wangu kwa mashindano  makubwa kama haya
  • Kuwepo kwa mipango endelevu ya kuhakikisha  kuna kuwapo na utaratibu mzuri wa kuendeleza vipaji vinavyo onekana kupitia michezo hii.
  • Kuwa husisha wadau wanao kuwa ni mhimili mkubwa katika michezo hii kamaWaamuzi, Makocha, Madakitari n:k
  • Kuchanganya michezo anuai ilikuhusisha jamii kwa ujumla wake zaidi ya wale wanaocheza soka. (Kuwepo na Netiboli, Voleboli, Mpirawakikapu na hata wa Mpirawamikono)
  • Kuwepo kwa mikakati kabambe inayolenga vijana wadogo zaidi kuliko watu wazima ambao hata ufundishaji wake muda mwingine ni mgumu.
kwaujumla jitihada zilizo tumika kwa  kuandaaa michezo hii ni zakuunga  mkono na kuboresha katika maandalizi yake kwa manufaa ya jamii na vizazi vijavyo.

Michezo ni Afya, Urafiki, Furaha, tena pia ni Ajira.
Picha juu gari la matangazo katika  michezo hiyo

Bwana Mpombo akizungumza na hadhira  juu ya umuhimu wa michezo hiyo

Katibu wa Chama cha mpira wa miguu  Mkoa wa Singida akifungua  michezo hiyo  Bw.Hussein Mwamba
Waamuzi wa michezo hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Wachezaji.
kamati ya ulinzi katika mashindano hayo

Changia mawazo yako hapa, Kuwa huru kuandika chochote kwa manufaa ya jamii
EmoticonEmoticon