Millionaire  Ads

Thursday, August 7, 2014

MUNGHANGA FOOTBALL ACADEMY ZA KWAANA VIKALI NA IBUN BUZ FOOTBALL CLUB UWANJA WA NAMFUA MJINI SINGIDA

Tags

lilikuwa ni pamabano la kuvutia baina ya timu mbili zilizo cheza jana jioni Uwanja wa mkoa wa Namfua. pambano hili lilihusisha timu mbili toka mjini singida ambazo ni Mughanga football Academy na Ibun buz. Pambano hili ni moja ya maandalizi  ya kujiandaa na Ligi ya Mkoa inayo tarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu 2014.Ligi hiyo itakuwa na dhumuni la kuweza kupata timu itakayo utetea mkoa wa Singida katika medali ya Soka dhidi ya mikoa mingine. Timu hizi zilimaliza mchezo ambapo Ibun bazi iliibuka na na ushindi wa goli moja kwa bila (Sifuri) dhidi ya Mughanga.
Nidhahili kwamba singida haija weza kupata timu mwakilishi wa Mkoa katika mashindano makubwa ya daraja la kwanza na ligi kuu kwa mda mrefu sasa. kuna maswali mengi pia ambayo bado hayaja patiwa majibu aidha kwa kukosekana majibu hayo au kwa kuwepo majibu yasiyo kuwa na mashiko vichwani mwa wadau.
Maswali haya nikama:-
  1. Kiko wapi kizazi kilicho utetea mkoa wa Singida ndani ya Singida United na kindai Shooting?
  2. Uko wapi uongozi ulio pigana kufa na kupona  miaka ya ushindi wa Taifa cup?
  3. Wako wapi wadau walio pandisha timu miaka ya Samaria ya Itigi?
  4. Uko wapi mpira uliochezwa enzi za Mto Fc?
lakini pia swali jingine linalo kuna vichwa wadau  ndani na nje ya Mkoa wa Signida ni lile la  uwepo wa viwanja vizuri kabisa  vyenye magoli ya kisasa kwa kila kijji kwa mkoa wote wa singida, Hali ambayo nifursa ya pekee kwa mkoa huu. Ipo haja sasa ya kupanga mikakati endelevu isiyo tanguliwa na maslahi binafsi itakayo tutoa hapa tulipo kutupeleka mahali pengine pazuri zaidi.
 Nafikiri sasa umefika wakati wa viongozi wa mpira wa miguu Mkao kushirikiana na serikali ya mkoa kuwekeza mawazo, Muda na Mali katika michezo kwani Singida ni moja ya mikoa inayo weza kunufaika sana na Ajira kupitia michezo kuliko mikoa mingine  ikutokana na fursa zilizopo, asili na historia ya mkoa, hali ya hewa pamoja na uwepo wa wadau waliowekeza katika eneo la michezo.
kwa mfano Mradi wa michezo wa TTU-Education Through Sports Singida, Miradi mingi ya michezo inayo fadhiliwa na Mh.Mbunge Bwana  Mohamed Dewji (Mo cup).

Wachezaji wa Mughanga Football academy Ibun Buz Footbal Club  wanasaliamiana tayari kwa kuanza mchezo.

Mwl. Abdallah Mwinyimkuu katikati ndiye muamzi wa mchezo huu akisaidiwa na Muamzi wa kwanza kushoto kwake  Fredrick Ndahani  na pia kulia kwake ni mwamzi msaidizi Pili Deusi


vijana  wako tayari kwa kuanza mchezo timu zote mbili



waamuzi wakisalimiana na makapteni wa timu zote mbili

Waamuzi wakitambaulishana na makepteni wa timu na kuelekezana utaratibu wa mchezo.

1 comments so far

Waliovutiwa na habari zako nzuri lazima watakomenti tu kama mimi ninavyo komenti hapa.

Changia mawazo yako hapa, Kuwa huru kuandika chochote kwa manufaa ya jamii
EmoticonEmoticon