Millionaire  Ads

Monday, August 18, 2014

MAANDALIZI YA MICHEZO YA COPA COCACOLA KUENDELEA MKOANI SINGIDA.

Tags

Ni maandalizi ya timu zinazo shiriki  michuano ya copa cocacola amabayo inayotarajiwa kutimua vumbi  kwa ngazi ya mkoa si siku nyingi.Kwa sasa kila wilaya imekwisha fanya mchakato wa kuona zina pata timu itakayo wakilisha wilaya husika katika michezo hii. Akitoa ufafanuzi katibu wa chama cha mpira wa miguu halmashauri ya Manispaa ya Singida (SIDIFA) Bw. Hamis kitila amaesema  wamefanya ung'amuzi wa vipaji kutokana na michuano iliyofanyika wiki iliyopita ambapo tayari wameshapata timu ambayo itawakilisha  Manispaa ya Singida na sasa timu hii inaendelea na mazoezi katika viwanja vya mwenge na Namfua.
Sambamba na hilo Bw. kitila ameeleza kuwa kwa mwaka huu ushindani utakuwa mkubwa sana na anashauri viongozi wa wilaya nyingine ambazo ni Manyoni,Singida vijijini na Iramba kuzingatia umri ilikuleta ufanisi katika kile ambacho kimelengwa na wadhamini ambao ni kampuni ya Cocacola.
michezo hii imetoa fursa kubwa sana kwa vijana kwani vipaji vingi vinavyotokana namichezo hii vimetumika katika kuinua timu za mikoa na wilaya husika . wito kwa Wadau wote  tunaomba tuwape kipaumbele vijana hawa kwani ndio watakao unda timu ya taifa ya siku za mbeleni.
 vjana wakiwa mazoezini uwanja wa mkoa
 Mwl.mohammed kweka akifundisha vijana hawa
 kijana akifanya kile alichofundishwa na Mwalimu  wake
Mwl.Mohammed Kweka akielekeza jinsi ya kupokea na kutoa pasi

Changia mawazo yako hapa, Kuwa huru kuandika chochote kwa manufaa ya jamii
EmoticonEmoticon