JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TANZANIA
KUWA MWENYEJI WA MASHINDANO YA SHIRIKISHO LA MICHEZO YA SHULE ZA SEKONDARI AFRIKA MASHARIKI
Tanzania imepewa
heshima ya kuwa Mwenyeji wa mashindano ya Michezo ya shule za Sekondari Afrika Mashariki
yajulikanayo kama FEASSSA (Federation of
East Africa Secondary Schools Sports Association),ambayo yatafanyika
Jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 22 Agosti hadi 1 septemba mwaka huu 2014.
Wanachama wa
mashindano haya ni Wanafunzi wa shule za
sekondari kutoka Wizara zenye dhamana ya
elimu katika nchi wanachama wa Jumiya ya
Afrika Mashariki. Nchi hizo ni:-
NO.
|
NCHI
|
WACHEZAJI
|
VIONGOZI
|
JUMLA
|
|
WASICHANA
|
WAVULANA
|
||||
1.
|
Tanzania
Bara
|
310
|
270
|
120
|
700
|
2.
|
Tanzania
Zanzibar
|
34
|
70
|
15
|
119
|
3.
|
Uganda
|
422
|
393
|
89
|
904
|
4.
|
Rwanda
|
129
|
142
|
79
|
350
|
5.
|
Kenya
|
327
|
326
|
88
|
741
|
6.
|
South
Sudan
|
215
|
|||
7.
|
Burundi
|
208
|
41
|
249
|
|
JUMLA
|
Michezo
hii mikubwa katika Ukanda huu,inategemewa kukutanisha Wanamichezo zaidi ya 3000 (elfu tatu)
watakaoshiriki michezo ifuatayo:-
1.
Mpira wa Miguu-Wavulana na Wasichana
2. Mpira
wa Kikapu-Wavulana na Wasichana
3. Mpira
wa Wavu-Wavulana na Wasichana
4. Mpira
wa Mikono-Wavulana na Wasichana
5. Netiboli-Wasichana
6. Mpira
wa Meza –Wavulana na Wasichana
7. Riadha-Wavulana
na wasichana
8. Mpira
wa Magongo (Hockey)-Wavulana na Wasichana
9. Lawn
tennis- Wavulana na wasichana
10. Badminton-Wavulana
na Wasichana
11. Rugby-Wavulana
12. Kuogelea-Wavulana
na Wasichana
Madhumuni
ya FEASSSA ni kufanya mashindano ya michezo kwa Wanafunzi wa shule
za Sekondari kwa Nchi wanachama kwa
malengo ya kujenga mahusiano, ushirikiano, mshikamano, upendo na umoja miongoni
mwa vijana na raia wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kilele hiki hutoa
taswira ya chachu ya Michezo shuleni na maandaalizi ya timu za Taifa za Vijana
katika uwakilishi wa nchi zao.
Mashindano
yameendelea kufanyika kila mwaka tangu 2002, kwa mara ya kwanza yalifanyika
Nairobi nchini Kenya. Nchi Mwenyeji huteuliwa
na Kamati ya utendaji ya FEASSSA kwa kuangalia kukidhi vigezo vya uenyeji.
Tanzania ilikuwa Mwenyeji kwa mara ya mwisho 2006 Dar es salaam.
Viongozi mbali mbali kutoka nchi wanachama,
wataambatana na Wanamichezo wao kushiriki shughuli hii muhimu na kutoa fursa zingine
kama za kibiashara, kielimu, kiutamaduni na kiutalii kwa faida na manufaa ya
wananchi wetu.Ni fursa nzuri pia kuona ushirikiano wa Wizara zetu kama ya
Uhusiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo
nk. katika kuleta ufanisi wa Uenyeji huu.
Aidha,
viwanja vitakavyotumika katika michezo hii ni pamoja na:-
·
Uwanja wa Taifa ambapo licha ya
kutumika kwa ufunguzi na ufungaji wa mashindano, michezo ya netiboli, mpira wa kikono, mpira
wa wavu, mpira wa kikapu, mpira wa
na tennis itachezwa kwenye
viwanja vilivyochorwa kuzunguka eneo la uwanja huo
·
Viwanja vya Chuo Kikuu cha
Dar-es-salaam kwa michezo ya ruby, hockey na kuogelea
·
Viwanja vya Chuo cha Polisi kwa ajili ya mpira wa miguu
·
Jitegemee Sekondari viwanja vya mazoezi
·
Viwanja vya Twalipo
·
Uwanja ndani kwa ajili badminton
·
Uwanja wa karume mpira wa miguu
·
DUCE mpira wa miguu
Shule
za Tanzania zinazoshiriki mashindano hayo ni zile zilizofanya vizuri kwenye
mashindano mbalimbali yaliyofanyika hapa nchini ambazo ni:-
·
Makongo Sekondari ya Mkoa wa DSM
·
Lord Baden Powell ya Mkoa wa Pwani
·
Tirav Sekondari ya Mkoa wa DSM
·
Kilabela Sekondari ya Mwanza
·
Techford Sekondari ya Morogoro
·
Kizuka Sekondari ya Morogoro
·
Abdul Jumbe sekondari, Kigamboni DSM
·
Shule ya Wasichana Masasi , Mtwara
·
Popatlali Sekondari Tanga
·
Tanga Sekondari
·
Meliwa Sekondari, Dodoma
·
Iyunga Sekondari
Mashindano
haya yatafunguliwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete tarehe 24/08/2014 saa 8.00
mchana na kufungwa rasmi na Rais
wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Mohammed Shen tarehe 31/ 08/2014
saa 8.00 Uwanja wa Taifa na viongozi wa juu katika Taifa letu la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania wamealikwa kushiriki katika hafla hizo.
Vile
vile mabalozi wa nchi zinazoshiriki michezo hiyo wamealikwa kushiriki ufunguzi,
ufungaji na kuwa wageni wa heshima wakati wote wa mashindano hayo.
Tahadhari
zote za ulinzi na usalama wa watu na mali zimewekwa kupitia vikao mkakati
ambapo jeshi la polisi na usalama vimetoeushirikiano katika vikao kazi vyote
tulivyokaa kwa ajili ya kufanikisha mashindano haya. Hivyo, wananchi mnaomba
kujitokeza kwa wingi kuja kushuhudia na kushangilia timu zetu na vilevile kutia
hamasa ya michezo hii.
Timu
za kutoka nje ya Tanzania zinatarajiwa kuwasili tarehe 22/08/2014 kupitia Mtukula, Lusumo, Kakongo na Namanga. Timu zote zitakapowasili
Tanzania zitapumzika katika shule za Bishop
Durning sekondari ya Arusha na Mwenge Sekondari ya Singida.
Washindi
wa michezo hiyo watatunukiwa zawadi mbalimbali zikiwemo Medali na vikombe. Timu
yetu ya Tanzania imeweka kambi ya wiki moja katika Chuo Kikuu Kishiriki cha
DUCE.
Tunatoa
wito kwa watanzani wote na wapenda Maendeleo ya michezo kuona umuhimu wa
kuisaidia timu hii ili iweze kufanya vizuri zaidi katika mashindano haya.
KARIBUNI WOTE MTUUNGE
MKONO KUFANIKISHA TUKIO HILI KUBWA NA LA AINA YAKE.
Changia mawazo yako hapa, Kuwa huru kuandika chochote kwa manufaa ya jamii
EmoticonEmoticon