Millionaire  Ads

Thursday, August 28, 2014

MRADI WA TTU-EDUCATION THROUGH SPORTS WAGAWA VIFAA VYA MICHEZO KWA WALIMU WA MICHEZO 12 MKOA WA SINGIDA

Tags
Mradi unaoshughulika na maendeleo ya michezo mashuleni mkoa wa singida  unaojulikana kwa jina la TTU-education through sports umegawa vifaa vya michezo  kwa walimu wa michezo walio hudhulia mafunzo ya Mchezo wa Riadha kwa siku Tano katika ukumbi wa cha cha walimu mkoa wa Singida. vifaa hivyo ni .
mipira ya mikono( handball)
  • Visahani vya kurusha katika Riadha (Discus)
  • Mtufe ya kurusha katika Riadha ( Shot-put) 
  • Mikuki ya kurusha katika Riadha (Javelin)
vifa hivyo vilikabidhiwa kwa walimu hawa kwaniaba ya wilaya zao husika  Ambazo ni Halmashauri ya Manipaa ya Singida, Halmashauri ya Wilaya ya singida vijijini, Halmashauri yaWilaya ya Iramba, Halmashauri ya wilaya ya Ikungi, Halmashauri yaWilaya ya  Manyoni na Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama.
Vifaa hivyo vilikabidhiwa kwa walimu hao na Meneja wa mradi huo  mbele ya Mgeni rasim Bw.Henry kapera Afisa michezo wa Mkoa wa Singida na Maofisa wa wa Elimu wa wilaya husika. Sambamba na hilo Mwenyekiti wa Chama cha walimu Bw. Alan Jumbe ambaye pia ni Mwenyekiti wa bodi ya mradi huu alishauri sana kuwa vifaa hivyo ni jitihada za chama na wadau kwaajiri ya kuhakikisha michezo na elimu vinakwenda sambamba hasa katika shule  kwani shule ndizo zilizo sheheni vipaji vya kila namna vya michezo hivyo  chama kitahakikisha kupitia mradi huu unasambaa kwa nchi nzima ikibidi, kwani michezo imechochea sana mahudhurio katika shule lakini pia imeimarisha utimamu wa afya za wanafunzi  katika shule na kuwafanya wasome vizuri bila kuwa na mteteleko wa kiafya.
 
  Mwenyekiti wa chama cha walimu Mkoa wa singida ambaye pia ni Mwenyekiti wa mradi  akiwa kushot kwa mgeni rasimi wakiwa na kaimu katibu wa mkoa wa Singida  kwanza kshot kwa mgeni rasimi aliye simama
Mgeni rasm Bw.Henry Kapera akiwa anatoa maelezo juu ya mafunzo haya tangu kuanza hadi mwisho wake

 Meneja wa mradi akiwagawia Walimu wa Michezo vifaa pamoja na Maafisa wa Elimu kutoka kila wilaya.
 Maafisa wa Elimu wakiwa navifaa vya Michezo  ambavyo ni Mikuki, Visahani, Matufe na Mipira

 Walimu na Maafisa Elimu Wakiwa wamebeba vifaa husika katika picha

Monday, August 25, 2014

TIMU YA VETERAN SINGIDA YA ENDELEA KUJINOA.

Tags
Mojawapo ya timu ambazo zinafanya mazoezi kwa juhudi na kwa ratiba maalumu kwa mkoa wa Singida ni timu ya  Veteran Singida Timu ambayo imedumu kwa muda mrefu sasa tangu kuanzishwa kwake.
Timu hii inaundwa na Waamuzi, Makocha na Wachezaji waliostaafu soka kwa miaka kadha iliyopita, kwa hivyo timu hii imesheheni kila aina ya watu ambao wanaujuzi katika soka  kwani  mchezaji asipokuwa alikuwa Muamzi basi atakuwa alikuwa kocha na kama hakuwa kocha basi atakuwa alikuwa mchezaji hivyo Veteran hawa wamekuwa  mchango mkubwa  katika maendeleo ya michezo hasa mpira wa miguu.
Timu hii pamoja na malengo hayo mazuri  bado wadau walikuwa wanashauri kuwa itakuwa vema endapo itatumika kama Timu ya mafunzo  kwa wadau wa mpira wa miguu kwakuwa  kuna uwezekano mkubwa sana timu nyimgine zikawa zinajifunza kupitia timu hiyo kwa mfano.
  • Veterani ambao ni makocha wanaweza kuwafundisha wachezaji wengine toka timu nyingi namna nzuri ya kucheza mpira kwani asilimia kubwa za maveterani hawa walifanya vizuri enzi zao  wakiwa wanacheza, wanafundisha au wanachezesha mpira.
  • lakini pia maveterani ambao wamekuwa waamuzi wa muda mrefu wanaweza wakasaidi timu nyingine namna ya kutafsili sheria hali itakayo saidia timunyingine kucheza mchezo mzuri usiokuwa na makosa mengi  na ya mara kwa mara.
  • Upande wa wachezaji  wa timu hii wangesaidi kushauri timu nyingine maswala mazima ya nidhamu, Uzalendo, juhudi na ujasisili wa kutetea timu yao pindi wanapo kuwa mchezoni.
Mimi nafikiri hii itakuwa namna nzuri ya kuboresha timu zetu iliziweze kufanya vizuri katika michezo yake tofauti na sasa ambavyo timu hizi zimekuwa zikisusua sana katika mashindano
Ninashauri pia veterans wote kuwa karibu sana na timu hizi ambazo zinaibukia na kukosa mwelekeo baadaye.

 Timu ya veterani ikiwa katika mazoezi siku ya Jumamosi
 Mchezaji wa veterani akionesha ufundi wake katika kucheza  Soka
 Wachezaji wakijaribu kutumia mbinu tofauti tofauti katika kupiga na kupokea pasi .
 Timu ya veterani ikiwa katika mazoezi siku ya Jumamosi
 Timu ya veterani ikiwa katika mazoezi siku ya Jumamosi
Vijana hawa wazamani wakioneshana ufundi katika kupokea na kuumiliki mpira  sawia 

Friday, August 22, 2014

Tags

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

                                                                TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MASHINDANO YA SHIRIKISHO LA MICHEZO YA  SHULE ZA SEKONDARI  AFRIKA MASHARIKI
Tanzania imepewa heshima ya kuwa Mwenyeji wa mashindano ya Michezo  ya shule za Sekondari Afrika Mashariki yajulikanayo kama FEASSSA (Federation of East Africa Secondary Schools Sports Association),ambayo yatafanyika Jijini  Dar es salaam kuanzia  tarehe  22 Agosti  hadi 1 septemba mwaka huu 2014.
Wanachama wa mashindano haya ni  Wanafunzi wa shule za sekondari kutoka  Wizara zenye dhamana ya elimu  katika nchi wanachama wa Jumiya ya Afrika Mashariki. Nchi hizo ni:-

NO.
NCHI
WACHEZAJI
VIONGOZI
JUMLA
WASICHANA
WAVULANA
1.
Tanzania Bara
310
270
120
700
2.
Tanzania Zanzibar
34
70
15
119
3.
Uganda
422
393
89
904
4.
Rwanda
129
142
79
350
5.
Kenya
327
326
88
741
6.
South Sudan



215
7.
Burundi
                     208
41
249
JUMLA
3,178

Michezo hii mikubwa katika Ukanda huu,inategemewa kukutanisha  Wanamichezo zaidi ya 3000 (elfu tatu) watakaoshiriki michezo ifuatayo:-
1.    Mpira wa Miguu-Wavulana na Wasichana
2.    Mpira wa Kikapu-Wavulana na Wasichana
3.    Mpira wa Wavu-Wavulana na Wasichana
4.    Mpira wa Mikono-Wavulana na Wasichana
5.    Netiboli-Wasichana
6.    Mpira wa Meza –Wavulana na Wasichana
7.    Riadha-Wavulana na wasichana
8.    Mpira wa Magongo (Hockey)-Wavulana na Wasichana
9.    Lawn tennis- Wavulana na wasichana
10. Badminton-Wavulana na Wasichana
11. Rugby-Wavulana
12. Kuogelea-Wavulana na Wasichana
Madhumuni ya  FEASSSA ni kufanya  mashindano ya michezo kwa Wanafunzi wa shule za Sekondari  kwa Nchi wanachama kwa malengo ya kujenga mahusiano, ushirikiano, mshikamano, upendo na umoja miongoni mwa vijana na raia wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kilele hiki hutoa taswira ya chachu ya Michezo shuleni na maandaalizi ya timu za Taifa za Vijana katika uwakilishi wa nchi zao.
Mashindano yameendelea kufanyika kila mwaka tangu 2002, kwa mara ya kwanza yalifanyika Nairobi nchini Kenya. Nchi Mwenyeji  huteuliwa na Kamati ya utendaji ya FEASSSA kwa kuangalia kukidhi vigezo vya uenyeji. Tanzania ilikuwa Mwenyeji kwa mara ya mwisho 2006 Dar es salaam. 
Viongozi  mbali mbali kutoka nchi wanachama, wataambatana na Wanamichezo wao kushiriki shughuli hii muhimu na kutoa fursa zingine kama za kibiashara, kielimu, kiutamaduni na kiutalii kwa faida na manufaa ya wananchi wetu.Ni fursa nzuri pia kuona ushirikiano wa Wizara zetu kama ya Uhusiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo nk. katika kuleta ufanisi wa Uenyeji huu.                           
Aidha, viwanja vitakavyotumika katika michezo hii ni pamoja na:-
·         Uwanja wa Taifa ambapo licha ya kutumika kwa ufunguzi na ufungaji wa mashindano,  michezo ya netiboli, mpira wa kikono, mpira wa wavu, mpira wa kikapu, mpira wa  na  tennis itachezwa kwenye viwanja vilivyochorwa kuzunguka eneo la uwanja huo
·         Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam kwa michezo ya ruby, hockey na kuogelea
·         Viwanja vya Chuo cha Polisi  kwa ajili ya mpira wa miguu
·         Jitegemee Sekondari viwanja vya mazoezi
·         Viwanja vya Twalipo
·         Uwanja ndani kwa ajili badminton
·         Uwanja wa karume mpira wa miguu
·         DUCE mpira wa miguu
Shule za Tanzania zinazoshiriki mashindano hayo ni zile zilizofanya vizuri kwenye mashindano mbalimbali yaliyofanyika hapa nchini ambazo ni:-
·         Makongo Sekondari ya  Mkoa wa DSM
·         Lord Baden Powell ya Mkoa wa Pwani
·         Tirav Sekondari ya Mkoa wa DSM
·         Kilabela Sekondari ya Mwanza
·         Techford Sekondari ya Morogoro
·         Kizuka Sekondari ya Morogoro
·         Abdul Jumbe sekondari, Kigamboni DSM
·         Shule ya Wasichana Masasi , Mtwara
·         Popatlali Sekondari Tanga
·         Tanga Sekondari
·         Meliwa Sekondari, Dodoma
·         Iyunga Sekondari
Mashindano haya yatafunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete tarehe 24/08/2014 saa 8.00 mchana na kufungwa  rasmi  na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Mohammed Shen tarehe 31/ 08/2014 saa 8.00 Uwanja wa Taifa na viongozi wa juu katika Taifa letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamealikwa kushiriki katika hafla hizo.
Vile vile mabalozi wa nchi zinazoshiriki michezo hiyo wamealikwa kushiriki ufunguzi, ufungaji na kuwa wageni wa heshima wakati wote wa mashindano hayo.
Tahadhari zote za ulinzi na usalama wa watu na mali zimewekwa kupitia vikao mkakati ambapo jeshi la polisi na usalama vimetoeushirikiano katika vikao kazi vyote tulivyokaa kwa ajili ya kufanikisha mashindano haya. Hivyo, wananchi mnaomba kujitokeza kwa wingi kuja kushuhudia na kushangilia timu zetu na vilevile kutia hamasa ya michezo hii.
Timu za kutoka nje ya Tanzania zinatarajiwa kuwasili tarehe 22/08/2014 kupitia Mtukula, Lusumo, Kakongo na Namanga. Timu zote zitakapowasili Tanzania zitapumzika katika shule za Bishop Durning sekondari ya Arusha na Mwenge Sekondari ya Singida.
Washindi wa michezo hiyo watatunukiwa zawadi mbalimbali zikiwemo Medali na vikombe. Timu yetu ya Tanzania imeweka kambi ya wiki moja katika Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE.
Tunatoa wito kwa watanzani wote na wapenda Maendeleo ya michezo kuona umuhimu wa kuisaidia timu hii ili iweze kufanya vizuri zaidi katika mashindano haya.
KARIBUNI WOTE MTUUNGE MKONO KUFANIKISHA TUKIO HILI KUBWA NA LA AINA YAKE.

Thursday, August 21, 2014

KNOW THE REAL LOCATION OF SINGIDA REGION-TANZANIA

Tags


Singida is among of 25 Tanzania mainland region which is in central zone of Tanzania where in east bordered by Manyara Region, west bordered by Tabora region, north Shinyanga and South bordered by Mbeya and Dodoma Regions. The Region comprised six districts council which are Manyoni Ikungi Singida Rural, Singida Municipal, Iramba and Mkalama. Presently the Region has an area of 49,438 kmsq
Link of Singida Region location click here (https://www.google.co.za/maps/mm?authuser=0&hl=en)
1.   Population
According to 2012 National Census Report, Singida has a total population of 1,370,637 of where by 677,995 are male and 692,642 female with an increase rate of 2.3. % per annum But, almost_367,268 who are equal to 27% are children who under 18 years. Since a long times Singida remain in among of region which covered by extremely poverty due to historical and topographical reason where Singida didn’t produced  any specific cash crop which enabled the community to engage with it  for their development. But not now where they introduced the sunflower and Onion production which growing day to day.
Due to the fact that Singida region  is also among of few regions which got lucky to have the Railway and Main tarmac road across toward western and southern Countries such as Rwanda, Burundi, Democratic republic of Congo, Uganda and Sudan. Not only that but also that infrastructures (railway and Tarmac road) used by some region like Tabora, Kigoma, Rukwa,  Shinyanga,  Mwanza, Geita, Kagera, Mara  and Simiyu. 
that is short background  of Singida region Welcome Singida
The population of people living in Singida Region is available on this link (http://www.nbs.go.tz/sensa/index2.html)

 Kinyamwenda Rift valley's  Rocks
 Rift valley at kinyamwenda Easten part of Singida
Good vegetation   around kinyamwenda Rift valley
 Kindai lake
 Attractive area at Kindai lake
 Lake Singidani
 Good place for visiting at  singidani lake
Moreover for any one who are interest to visit singida   stay in touch with us for more instruction and logistics as well. 
Amani mwaipaja 
Box 392
Singida-Tanzania 
+255756219292
E-mail. mwaipajaamani@ymail.com
           mwaipajaamani@gmail.com
Skype.Amani.mwaipaja

                               welcome