Kutokana na mikakati inayo fanywa na chama cha waamuzi wa mpira wa miguu mkoani Singida (FRAT) kumekuwa na utaratibu kabambe ulio ratibiwa na Waamuzi wa ligi Kuu na FIFA wanaotoka Mkoa wa Singida. Chama hiki kimekuwa mfano wa kuigwa mkoani Singida. ubora huu umetokana na waamuzi kuwa na vipindi vya kufanya mazoezi kwa pamoja na pia kukaa na kupitia sheria Kumi na saba za soka kwa pamoja pia hali imepelekea chama hiki kiwe na mshikamano mzuri sana.
Wadau wa Mpira pia wameenda mbali kwa kupongeza uongozi wa chama cha waamuzi wa soka na Chama cha Mpira Mkoa wa Singida.
Ikumbukwe pia chama hiki mwanzoni mwa mwaka kilipatwa pigo la kuondokewa na Mwanyekiti wachama hayati Bw.Josephati Magazi ambaye pia alikuwa mkufunzi mkuu wa Wawaamuzi wa mpira wa miguu kwa mkoa wa Singida na Mechi Kamishina wa ligi kuu kwa zaidi ya miaka kumi na mbili, hata hivyo kutokana na miongozo yake mizuri waamuzi wameendelea kumuenzi kwa kushikamana na kuendelea kuwa wamoja na wenye nia ya kuhakikisha wanakuwa wadau halali wa mpira wa miguuua kwa kufuata miongozo na kanuni zinazo simamia chama.
kwa hili hongera chama cha Waamuzi mkoa wa singida na hongera waamuzi wa ligi kuu na FIFA kwa kuwa msitari wa mbele kuwaongoza waamuzi wenzenu na kuwa saidia kimazoezi.
Waamuzi wa mpira wamiguu Mkoa wa Singida wakiwa katika majadiano baada ya mazoezi siku ya Juma mosi katika uwanja wa mkoa wa Namfua Singida.
Waamuzi wa mpira wa miguu wakiwa katika zoezi la kuunyosha mwili baada ya mazoezi
Picha juu ni Darasa la waamuzi wa mpira wa miguu Mkoa wa Singida wakiwa katika mafunzo ya sheria kumi na saba za soka chini ya wa kiongozwa na Mwl. Arnold Bugado ambaye pia ni Mwamzi wa daraja la kwanza na anachezesha michezo ya Ligi kuu Tanzania bara.