Millionaire  Ads

Thursday, August 28, 2014

MRADI WA TTU-EDUCATION THROUGH SPORTS WAGAWA VIFAA VYA MICHEZO KWA WALIMU WA MICHEZO 12 MKOA WA SINGIDA

Mradi unaoshughulika na maendeleo ya michezo mashuleni mkoa wa singida  unaojulikana kwa jina la TTU-education through sports umegawa vifaa vya michezo  kwa walimu wa michezo walio hudhulia mafunzo ya Mchezo wa Riadha kwa siku Tano katika ukumbi wa cha cha walimu mkoa wa Singida. vifaa hivyo ni .
mipira ya mikono( handball)
  • Visahani vya kurusha katika Riadha (Discus)
  • Mtufe ya kurusha katika Riadha ( Shot-put) 
  • Mikuki ya kurusha katika Riadha (Javelin)
vifa hivyo vilikabidhiwa kwa walimu hawa kwaniaba ya wilaya zao husika  Ambazo ni Halmashauri ya Manipaa ya Singida, Halmashauri ya Wilaya ya singida vijijini, Halmashauri yaWilaya ya Iramba, Halmashauri ya wilaya ya Ikungi, Halmashauri yaWilaya ya  Manyoni na Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama.
Vifaa hivyo vilikabidhiwa kwa walimu hao na Meneja wa mradi huo  mbele ya Mgeni rasim Bw.Henry kapera Afisa michezo wa Mkoa wa Singida na Maofisa wa wa Elimu wa wilaya husika. Sambamba na hilo Mwenyekiti wa Chama cha walimu Bw. Alan Jumbe ambaye pia ni Mwenyekiti wa bodi ya mradi huu alishauri sana kuwa vifaa hivyo ni jitihada za chama na wadau kwaajiri ya kuhakikisha michezo na elimu vinakwenda sambamba hasa katika shule  kwani shule ndizo zilizo sheheni vipaji vya kila namna vya michezo hivyo  chama kitahakikisha kupitia mradi huu unasambaa kwa nchi nzima ikibidi, kwani michezo imechochea sana mahudhurio katika shule lakini pia imeimarisha utimamu wa afya za wanafunzi  katika shule na kuwafanya wasome vizuri bila kuwa na mteteleko wa kiafya.
 
  Mwenyekiti wa chama cha walimu Mkoa wa singida ambaye pia ni Mwenyekiti wa mradi  akiwa kushot kwa mgeni rasimi wakiwa na kaimu katibu wa mkoa wa Singida  kwanza kshot kwa mgeni rasimi aliye simama
Mgeni rasm Bw.Henry Kapera akiwa anatoa maelezo juu ya mafunzo haya tangu kuanza hadi mwisho wake

 Meneja wa mradi akiwagawia Walimu wa Michezo vifaa pamoja na Maafisa wa Elimu kutoka kila wilaya.
 Maafisa wa Elimu wakiwa navifaa vya Michezo  ambavyo ni Mikuki, Visahani, Matufe na Mipira

 Walimu na Maafisa Elimu Wakiwa wamebeba vifaa husika katika picha

Monday, August 25, 2014

TIMU YA VETERAN SINGIDA YA ENDELEA KUJINOA.

Mojawapo ya timu ambazo zinafanya mazoezi kwa juhudi na kwa ratiba maalumu kwa mkoa wa Singida ni timu ya  Veteran Singida Timu ambayo imedumu kwa muda mrefu sasa tangu kuanzishwa kwake.
Timu hii inaundwa na Waamuzi, Makocha na Wachezaji waliostaafu soka kwa miaka kadha iliyopita, kwa hivyo timu hii imesheheni kila aina ya watu ambao wanaujuzi katika soka  kwani  mchezaji asipokuwa alikuwa Muamzi basi atakuwa alikuwa kocha na kama hakuwa kocha basi atakuwa alikuwa mchezaji hivyo Veteran hawa wamekuwa  mchango mkubwa  katika maendeleo ya michezo hasa mpira wa miguu.
Timu hii pamoja na malengo hayo mazuri  bado wadau walikuwa wanashauri kuwa itakuwa vema endapo itatumika kama Timu ya mafunzo  kwa wadau wa mpira wa miguu kwakuwa  kuna uwezekano mkubwa sana timu nyimgine zikawa zinajifunza kupitia timu hiyo kwa mfano.
  • Veterani ambao ni makocha wanaweza kuwafundisha wachezaji wengine toka timu nyingi namna nzuri ya kucheza mpira kwani asilimia kubwa za maveterani hawa walifanya vizuri enzi zao  wakiwa wanacheza, wanafundisha au wanachezesha mpira.
  • lakini pia maveterani ambao wamekuwa waamuzi wa muda mrefu wanaweza wakasaidi timu nyingine namna ya kutafsili sheria hali itakayo saidia timunyingine kucheza mchezo mzuri usiokuwa na makosa mengi  na ya mara kwa mara.
  • Upande wa wachezaji  wa timu hii wangesaidi kushauri timu nyingine maswala mazima ya nidhamu, Uzalendo, juhudi na ujasisili wa kutetea timu yao pindi wanapo kuwa mchezoni.
Mimi nafikiri hii itakuwa namna nzuri ya kuboresha timu zetu iliziweze kufanya vizuri katika michezo yake tofauti na sasa ambavyo timu hizi zimekuwa zikisusua sana katika mashindano
Ninashauri pia veterans wote kuwa karibu sana na timu hizi ambazo zinaibukia na kukosa mwelekeo baadaye.

 Timu ya veterani ikiwa katika mazoezi siku ya Jumamosi
 Mchezaji wa veterani akionesha ufundi wake katika kucheza  Soka
 Wachezaji wakijaribu kutumia mbinu tofauti tofauti katika kupiga na kupokea pasi .
 Timu ya veterani ikiwa katika mazoezi siku ya Jumamosi
 Timu ya veterani ikiwa katika mazoezi siku ya Jumamosi
Vijana hawa wazamani wakioneshana ufundi katika kupokea na kuumiliki mpira  sawia