Millionaire  Ads

Friday, August 8, 2014

BAADHI YA PICHA WAKATI WAUGAWAJI WA ZAWADI TAMASHA LA MICHEZO KWA WALEMAVU.






Katika picha Meneja wa Mradi wa TTU-Education Through Sports ni Mwenye fulana nyekundu akiwakabidhi Walimu na Wanafunzi Zawadi.

MRADI USIO WA KISERIKALI WA TTU-EDUCATION THROUGH SPORTS WAENDESHA TAMASHA LA MICHEZO KWA WANAFUNZI WALEMAVU.

Wanafunzi zaidi ya miamoja  viziwi kutoka Shule ya Msingi ya Tumaini  iliyopo Manispaa ya Singida wameshiriki katika tamasha la michezo lililoendeshwa na Mradi usio wakiserikali wa TTU-Education Through Sports  Mradi unao husika  na maendeleo ya michezo Mkoa wa Singida.
Michezo iliyo husishwa katika tamasha hilo ni Riadha  Wavulana na Wasichana ambapo walikimbia na kutupa, Mpira wa Miguu Wavulana na Wasichina na Mpira wa Wawavu ambapo nao walicheza   wavulana na wasichana.
katika hali isiyo ya kawaida wanafunzi hawa walifurahi sana hali iliyowapelekea hata kutaka kuendelea na mchezo licha ya muda wakucheza kuwa umeisha.
 Mwalinu Mkuu wa shule hii Bw. Francis alikili kuwa wanafunzi wamefurahi sana hatawakakataa kwenda kula pindi muda wakula ulipowadia.
Akizungumza na wanafunzi wakiwa na Walimu wao, Meneja wa Mradi  wa TTU-Education Through Sports Bw. Arnold Bugado alisema kuwa Mradi umekuwa ikijitahidi kuishawishi jamii pamoja na wadau ilikuona watoto walemavu wanahusishwa katika michezo kikamilifu.pia alisema sehemu nyingi utakapokuta michezo ikifanyika  ni mara chache sana kukuta ikiwashirikisha walemavu, hivyo basi ni dhahiri kuwa kundi hili limesahaulika sana katika jamii yetu.
Meneja aliendelea kuwasihi walimu kuwa wavumilifu  na kuendelea na moyo ambao wamekuwa nao kwani  muda mwingi wamekuwa wakiutumia kuwalea watoto walemavu na kuwafundisha.
Shule ya msingi Tumaini  ni shule ambayo imejikita na ufundishaji wa Wanafunzi Viziwi (wasiosikia wala kuaongea) lakini pia shule hii imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi kama vile Msukumo mdogo kutoka kwa jamii, kutokuwapo na Mabweni ya wanafunzi na uchache wa vifaa vyakujifunzia na kufundishia  vilivyo maalumu kwa wanafunzi wenye ulemavu huo.
Mradi wa TTU- Education Through Sports  ulitoa zawadi kwa wanafunzi hao ikiwa ni pamoja na Jezi za michezo anuai, viatu vya mpira  na vya mazoezi, Mifuko midogo ya kuwekea vifaa vya shule na zawadi nyingine nyingi.
 Tunawashukuru Uongozi wa Mradi huo kwa kujitolea kwao.





Karibu utuambie  sehemu uliyoko kundi hili lina nafasi gani katika michezo.