Millionaire  Ads

Monday, April 3, 2017

Uzalendo na utaifa vinajengwa na viongozi wakubwa sio wananchi kama tunavyofikiria

Neno uzalendo linahubiriwa sana  kwa vijana wa Tanzania. Viongozi wakubwa wanahubiri hivyo. Lakini ukweli ni kwamba uzalendo unaanza kujengwa na viongozi wa ngazi za juu Kama marais, mawaziri, wabunge, kwakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya pamoja na viongozi wengine ambao ni wafanyakazi wa serikali wa kuajiriwa.


Ni vigumu kijana kuipenda nchi yake kama kijana huyu anashindwa kupata ajira, kijana huyu akienda sokoni vitu bei juu, Kijana huyu hata sehemu ya kulala kwake ni shida. Tuchukulie mfano Baba wa familia akihubiri uzalendo kwa watoto wake wakati watoto hawafurahii maisha jinsi yanavyoendeshwa kwenye familia hiyo.  Vijana hawa hata wakihubiriwa uzalendo mara elfu moja hawawezi kuwa na uzalendo na familia yao.

Uzalendo ni "involuntary action" Uzalendo unakuja automatically bila kulazimishwa au kusisitizwa na viongozi. Matendo vya viongozi kwa wananchi wao ndiyo yatakayowafanya wanachi kuwa na uzalendo au wasiwe na uzalendo. Kama viongozi watakuwa mafisadi, hawatendi haki sawa kwa wote pamoja na maovu mengine yanayoonekana na yasiyoonekana basi jamii wanayoiongoza lazima nayo ikose uzalendo.

Uzalendo ni kama upendo ukimpenda mtu naye atakupenda. Ukimwonesha uzalendo mwanachi basi naye mwananchi ataonesha uzalendo kwako hatimaye kitendo hiki kitajenga uzalendo kwa Taifa zima. Kama wananchi wanalalamikia uongozi uliopo madarakani kwa masuala mbalimbali kama vile kutosaidiwa kujikwamua kwenye wimbi la umaskini ni dhahirii kuwa wananchi nao hawatakuwa na uzalendo na serikali yao pamoja na taifa kwa ujumla.

Hayati mwalimu Julius kambarage nyerere alionesha uzalendo mkubwa kwa Taifa la Tanzania pamoja na Raia wa Tanzania ndio maana vijana wa muda huo walikuwa tayari hata kuifia nchi yao. Lakini leo hii sina uhakika kama vijana asilimia ngapi wanaweza kuitetea Tanzania ipasavyo kwa lugha nyingine kuwa na uzalendo. Kama kijana yupo tayari aende china akanunue bidhaa feki zenye madhara kwa Taifa la Tanzania ilimradi ajikwamue kiiuchumi baada ya kushindwa kufanikiwa kwa njia halali nchini mwake hii ni dalili ya kupoteza uzalendo. Viongozi tuna jukumu la kuwasaidia vijana hawa waweze kufanikiwa kwa kutumia fulsa halali zilizopo nchini mwao.

Tujitathmini je Sekta ya biashara ni rafiki kwa mfanyabiashara je sekta ya kilimo nayo ipo sawa? ni kweli kijana akisomea kilimo akaenda benki kukopa mtaji na kuwekeza kwenye kilimo atafanikiwa na kutengeneza ajira kwa vijana wengine? Haya ni baadhi tu ya maswali ya kujiuliza. Hapa ndipo Kiongozi unatakiwa kuumiza kichwa kutengeneza mazingira mazuri kwa wananchi wako toka moyoni sio tu kwa kuonekana kwenye Taarifa za habari.

Mwajiri umeajiri wafanyakazi kwenye taasisi yako anza wewe kuonesha uzalendo wajali wafanyakazi wako ili nao wajali taasisi yako. Ukibaki kutumia motivation za adhabu ukidhani ndo unawarekebisha watumishi wako ili upate matokeo mazuri inaweza kuwa kinyume chake. Uzalendo wa taasisi yako unaanza na wewe mkurugenzi wa taasisi husika, sio kwa kuwahubiria wafanyakazi wako kuwa wapende taasisi yako wapendende kazi wanazofanya kwenye taasisi yako wakati wewe huwapendi.

Baba wa familia ukitumia ubabe kuongoza familia yako basi utapata heshima za woga za ndiyo mkuu wakati upande wa pili wa pazia wanafamilia hawatakuwa na mapenzi na familia hiyo kwaku hawajisikii toka moyoni kuwa na uzalendo na familia hiyo.

Tujifunze uzalendo ni nini? Vitu gani vinasababisha jamii kuwa na uzalendo na Taifa lake?

Thursday, March 30, 2017

Tumia simu yako kujiajiri kwa kuandika blog

Hii ni ajira ya muda wa ziada. Uandishi kwenye blog. Unapewa blog ya kuandika habari zako unazozipenda unaifanya blog yako ijulikane na watu duniani kisha kila mwisho wa mwezi unakuwa unalipwa kwa kila anayesoma blog yako.

Kazi hii unaweza kuifanya kwa kutumia simu ya smartphone sio lazima uwe na kompyuta. Malipo ni mazuri sana. Hutajutia kufanya kazi hii yao uandishi kwenye blog. Unaweza kutuma maombi yako na kupewa blog leo hii hii tuma sms whatsap au telegram au wasapu kwa namba hii 0652428852

Je unaweza kuandika nini kwenye blog ili watu waipende na kuitembelea kila siku?

Hili ni swali zuri na ndiyo chanzo cha mafanikio kwenye kazi hiii ya uandishi wa blog.
Vipo vitu vingi vya kuandika ambavyo watu wanapendelea kuvitafuta kwenye mitandao kama blogs. Baadhi ya vitu hivyo ni kuandika habari zinazotangazwa kwenye vyombo vya habari kama Televisheni magazeti na redio unatakiwa uwe mfuatiliaji mzuri wa habari zinazungumziwa sana ndizo za kuandika kwenye blog yako. Mfano kama Rais Magufuli amezungumza kitu kuhusina na Mkuu wa mkoa wa Dar es salam na wiki hiyo habari nzito ilikuwa mkuu wa mkoa kupiga vita madawa ya kulevya basi tengeneza habari yenye uadilifu kutoka kwenye tukio hilo kisha andika kwenye blog yako muda si mrefu utakuta watu wanamiminika kwenye blog yako kutoka google search wakisoma habari hiyo. Angalizo tu usiiandike vibaya serikali au kiongozi wa serikali kwakua hakuna anayeweza kupambana na serikali hata kama awe na pesa namna gani. Kuwa mpole maisha yasonge mbele. Tafuta kipato chako achana na siasa inakupotezea muda japo ina mchango mkubwa katika kuboresha maisha yako lakini hakuna jinsi kwa nchi kama Tanzania.

Unaweza kuamua kufundisha mambo mbalimbali yahusuyo jamii kama jinsi ya kuendeleza kilimo cha kisasa, unaweza kuamua kufundisha masuala ya afya tu au kitu chochote ambacho una ujuzi nacho au kitu ulichosomea chuoni.

Je niandike habari ngapi kwa siku au kwa wiki?

Kisheria unapopewa blog unatakiwa kuandika habari zaidi ya tatu kwa wiki yaani kwa siku saba lakini kama unataka upate wasomaji wengi andika habari angalau moja kila baada ya saa moja au masaa mawili. Hizi ni habari unazozipata toka kwenye vyombo vya habari kama television au redio lakini kama umeamua kufundisha jamii mambo fulani unaweza andika makala moja kwa siku au kwa siku mbili. Ni vizuri uchanganye habari na matukio ya kila siku na makala za kufundisha jamii kitu unachokijua zaidi.


Je hiyo blog nayopewa naweza imiliki mpaka napozeeka?
Ndiyo unaimiliki kwa ngazi ya uandishi pia ukipata matangazo toka kwa watu wako tunakuwekea kwenye blog hiyo na pesa zote ni zako sisi hatuchukui hata shilingi kwakua tayari tuna matngazo yetu matatu kwenye blog hiyo. Unaimiliki blog maishani ili mradi tu usikiuke masharti ya uandishi ambayo unapewa siku ya kwanza unapopewa blog kama vile lazima uandike habari au makala si chini ya tatu ndani ya siku saba yaani kila wiki lazima uandike angalau habari tatu au makala tatu. kutofanya hivyo blog hiyo anapewa mwingine. Soma masharti yote na malipo kwa kubonyeza hapa

Tuma ujumbe sasa ukiwa whatsapp 0652428852 ukiwa telegram 0652428852 ukiwa kwenye mtandao wa wasapu 0652428852 elezea unataka kuandika mambo gani na unatoka mkoa gani wilaya gani. utajibiwa leo leo na kupewa blog leo leo.
Unaweza kuuliza wali hapa chini karibu sana